AGROBUSINESS
GO GREEN,CROP GO GRAINING MILLING , FOOD & BEVERAGE
Inajikita katika kilimo endelevu, uzalishaji wa mazao, na mbinu za kilimo rafiki
kwa mazingira ili kuongeza usalama wa chakula na kuhifadhi mazingira.
Pia inahusisha usindikaji wa nafaka, uzalishaji wa vyakula na vinywaji
kwa soko la ndani na kanda. Kupitia miradi hii, tunawaunganisha wakulima
wadogo na wa kati na masoko ya kisasa, kuongeza thamani ya mazao yao
na kuwapatia maarifa ya kilimo cha kisasa pamoja na teknolojia bora ili kuleta mapinduzi ya sekta ya kilimo.
BROAD CAST & MEDIA
GOLDEN TV HD, RADIO, MOVIE & DOCUMENTARY STUDIOS
Inalenga katika utoaji wa huduma za habari na burudani kupitia televisheni
za kisasa zenye chaneli nyingi, studio za picha, sinema na radio za mtandaoni
ili kukuza utamaduni, kutoa elimu, na kufikisha habari za maendeleo
kwa jamii. Tunapanua wigo wa mawasiliano kwa kutumia teknolojia ya kidigitali,
kuwahusisha vijana katika uzalishaji wa maudhui na kuhakikisha Tanzania
inaendelea kung’ara kwenye ramani ya vyombo vya habari Afrika.
LOGISTICS & TRANSPORT
GOLDEN CLEAVERY LUXURY TRANSPORT, MARINE & AVIATION
Hutoa huduma za usafirishaji za ardhini, majini na angani ikiwa ni pamoja
na miradi ya mabasi ya kisasa, bajaji, bodaboda, malori makubwa, boti za
kisasa na ndege za ndani. Tunarahisisha biashara, kuongeza mtiririko wa bidhaa,
na kuunganisha masoko ya mikoa na nchi jirani ili kuchochea uchumi wa kikanda
na kuongeza nafasi za ajira kwa watanzania.
HOSPITALITY & LEISURE
GOLDEN HOTELS, RESTAURANTS & PICNIC CENTERS
Inatoa huduma za malazi ya kifahari, migahawa yenye vyakula vya kimataifa
na vya asili pamoja na vituo vya mapumziko vinavyofaa kwa familia na
makundi ya kijamii. Kupitia sekta hii tunakuza utalii wa ndani, tunatengeneza
fursa nyingi za ajira na kutoa chaguo bora kwa wageni wanaokuja kutembelea
nchi yetu ili wajisikie kama wako nyumbani.
REAL ESTATE
APARTMENTS, COMMERCIAL BUILDINGS & PROPERTY AGENCY
Inawekeza katika ujenzi na usimamizi wa majengo ya vitega uchumi kama
apartments za kisasa, majengo ya biashara, na ofisi zinazokidhi viwango
vya kimataifa. Pia tunatoa huduma za udalali wa mali isiyohamishika kwa
kurahisisha mauzo na upangishaji. Lengo letu ni kuchangia ukuaji wa miji
na kutoa mazingira bora ya kuishi na kufanya biashara.
AVIATION & MARINE
AIRLINES, FERRIES, FAST BOATS & SHIP YARDS
Inajihusisha na uwekezaji katika usafirishaji wa angani na majini kwa
lengo la kufungua fursa za biashara na utalii wa kimataifa. Tunaboresha
viwango vya huduma kwa kutumia teknolojia mpya na kushirikiana na
wataalamu kutoka nchi mbalimbali ili kuhakikisha wateja wetu wanapata
usalama na huduma bora za usafiri wa anga na maji.
SECURITY & PRIVATE MILITARY
SECURITY SERVICES & HIGH TECH SYSTEMS
Hutoa huduma za ulinzi wa binafsi na mali kwa kutumia mifumo ya kisasa
ya kamera, sensa na vikosi maalum vilivyopata mafunzo ya kitaalam.
Tunasaidia kampuni, mashirika na watu binafsi kuimarisha usalama wao
katika mazingira ya biashara na makazi, huku tukizingatia kanuni za
kitaaluma na maadili ya hali ya juu.
SPORTS, HEALTH & EDUCATION
STADIUMS, SCHOOLS, HOSPITALS & ACADEMIES
Inajikita kwenye kuboresha afya, elimu na michezo kwa jamii kwa kujenga
viwanja vya michezo vya kisasa, shule za msingi hadi vyuo, hospitali na
academy za vipaji. Hii inawawezesha vijana kupata fursa za kuibua na
kuendeleza talanta zao, huku wakiishi maisha yenye afya bora na kupanua
maarifa yao.
MINING, GAS & PETROLEUM
EXTRACTION & DISTRIBUTION OF NATURAL RESOURCES
Inashughulika na uchimbaji wa madini, gesi na mafuta, pamoja na usambazaji
wake kwa viwanda na masoko ya ndani na nje ya nchi. Tunachochea
uzalishaji wa bidhaa za kuongeza thamani ya maliasili ili kuongeza mapato
kwa taifa na kutoa ajira nyingi kwa vijana na wakazi wa maeneo yanayozunguka migodi.
RESEARCH & INNOVATION
TECHNOLOGY, LABORATORIES & DEVELOPMENT PROJECTS
Inajihusisha na utafiti, uvumbuzi wa teknolojia mpya na maendeleo ya
miradi bunifu kwa sekta zote za uchumi. Tunashirikiana na taasisi za
kitaaluma na wabunifu chipukizi ili kuja na suluhisho za changamoto
zinazowakabili wakulima, wajasiriamali na mashirika mbalimbali.
ENGINEERING & I.C.T
CONSTRUCTION, MANUFACTURING & ICT SERVICES
Inasimamia miradi mikubwa ya ujenzi wa miundombinu, kuanzisha
viwanda vya kutengeneza bidhaa na kutoa huduma za ICT za kidigitali
kwa makampuni na jamii. Hii inarahisisha kazi zao za kila siku na kuongeza
ufanisi wa biashara zao, huku tukichochea ajira na ubunifu nchini.
MICROFINANCE & BANKING
MICRO LOANS, INVESTMENT SERVICES & COMMUNITY BANKING
Inatoa huduma za mikopo midogo kwa wakulima, wafanyabiashara na
wajasiriamali, huduma za uwekezaji pamoja na benki za jamii ili kuongeza
mtaji na kuinua uchumi wa mtu mmoja mmoja. Tunatoa ushauri na
elimu ya fedha kuhakikisha wateja wetu wanafanikiwa na kufanya biashara
zao kwa tija zaidi.